Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Salum Mwalimu amedai hawezi kwenda
Bungeni kuwa Mbunge wa CHADEMA bali yeye anataka kuwa Mbunge wa wananchi wote
bila ya kujali vyama vyao.
Salum Mwalimu ametoa kauli hiyo ikiwa yupo katika muendelezo
wa kuomba kura kwa wananchi wa Jimbo la Kinondoni ambao wanatarajia kuingia
katika chaguzi ndogo siku za hivi karibuni za kumtafuta Mbunge wanayemtaka
katika Jimbo lao ambalo kwa sasa lipo wazi.
"Siendi kuwa Mbunge wa CHADEMA bali naenda kuwa
Mbunge wa wananchi wa Kinondoni, nitakae watumikia kwa haki kila mmoja katika
jimbo hili. Pia ni kwamba sitokubali kuwa sehemu ya wasaliti wala unafki",alisema
Salum Mwalimu.
Aidha, Salum Mwalimu amesema anamatumaini tosha kuwa yeye
ndio atakae kuwa Mbunge mtarajiwa wa Jimbo hilo huku akidai hatarajii kuona
uchaguzi mdogo ukiwa unarudiwa kwa mara nyingine.
"Hatutarajii kuona uchaguzi mdogo mwingine hapa
labda Mwenyezi Mungu aliyenipa uhai achukue pumzi zake lakini siyo
vinginevyo", alisisitiza Salum.
Kwa upande mwingine, mgombea huyo amedai atatumia maarifa
yake yote aliyonayo ili aweze kuwaunganisha wananchi wa jimbo hilo na kuweza
kuzungumza pamoja katika kujenga maendeleo yao.
Post a Comment
karibu kwa maoni