Kufuatia ugonjwa Saratani ya mlango wa kizazi kuzidi kuwakumba wengi wao bila kujua hospitali ya mkoa wa Manyara imewataka Wanaume na na wanawake kujitokeza hospitalini hapo kupatiwa vipimo bila malipo yeyote.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara Bi. Catherine Magari na Dk.Stanley Makundi wakizungumza na WALTER HABARI wamesema kuwa ugonjwa huo wa Saratani ya mlango wa kizazi unasababishwa kwa kiwango kikubwa na kujamiiana na Vijidudu wanaojuliakana kitaalamu kama ‘Human papilloma virus’ au HPV na hauna uhusiano wowote na Virusi vinavyosababisha
Ukimwi [VVU].
Ukimwi [VVU].
Madaktariwanasema kuwa tatizo linapotokea huwa hakuna dalili kubwa za awali zaidi ya kutokwa na damu ukeni, maumivu ya nyonga na maumivu wakati wa tendo la ndoa, wakati mwingine damu inatoka baada ya tendo la ndoa.
Aidha mtu ambaye tayari alishawahi kupata maambukizi haya awali na akapona, hawezi kupata tena kwa kuwa tayari anakuwa ameshatengeneza kinga ya kudumu dhidi ya vijidudu hivi vya HPV.
SIKILIZA HAPA CHINI
SIKILIZA HAPA CHINI
Post a Comment
karibu kwa maoni