0

Mtu mmoja anaesemekana kuwa ni  daktari wa hospitali ya mkoa wa Manyara amenusurika kifo baada ya jiko la gesi alilokuwa akilitumia chumbani kwake kulipuka hali iliyopelekea moto mkubwa kuwaka katika chumba hicho.
Tukio hilo limetokea usiku wa Leo March 14.2018 katika mtaa wa Nyunguu mjini Babati.
Licha ya watu kujitokeza kumuokoa,aliendelea kujifungia chumbani kwake na kuwapiga walikuwa wakimpa msaada lakini wakafanikiwa kuuvunja Mlango na kumtoa mtu huyo ambaye alionekana amelewa.

Hata hivyo jeshi la zimamoto na uokoaji walifika kwa wakati katika eneo la tukio na kuuzima moto huo  na kumpeleka katika kituo cha polisi.

Tanesco walizima Umeme kwa dakika 20,toka saa 2;30 hadi saa 2:40 usiku huu kukwepa madhara  kutokea zaidi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top