Lissu
amebainisha hayo usiku wa kuamkia leo wakati alivyokuwa anawafahamisha
umma juu ya maendeleo ya afya yanavyoendelea huko alipo na kusema
anaendelea vizuri na matibabu na sasa anaweza kusimama kwa miguu yote
miwili bila ya msaada wa magongo ya kutembelea.
"Timu ya madaktari bingwa wa mifupa wanaonitibu, wamenitaarifu kwamba kasi ya mfupa wa juu ya goti kuunga ni ndogo sana na kwamba wasipoingilia kati na kurekebisha mfupa huo, itachukua muda mrefu sana kuunga na hata ukiunga baada ya huo muda mrefu, hautaunga kwa namna itakayoondoa hatari ya kuvunjika siku za mbeleni. Kwa sababu hizi, madaktari wangu wamependekeza kufanya operesheni nyingine kwenye mfupa wa juu ya goti la kulia", amesema Lissu.
Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa kusema "Niko kwenye mikono salama ya kitabibu. Madaktari wangu, Prof. Dr. Stefa Nijs na Prof. Dr. Willem-Jan Mertsemakers, ni madaktari bingwa wa mifupa wanaosifika barani Ulaya kwa utaalamu wao katika fani hiyo. Hivyo msiwe na hofu, Mungu wetu aliyeniwezesha kuwa hai sasa, ataendelea kutenda miujiza yake kupitia kwa madaktari bingwa hawa. Nitaendelea kuwataarifu maendeleo ya matibabu yangu kadri itakavyokuwa lazima na muhimu kufanya hivyo".
Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana tangu Septemba 7,2017 akiwa mkoani Dodoma, na kisha kupelekwa nchini Nairobi kwa matibabu na baada ya miezi 3 alipelekwa nchini Ubelgiji kwa hatua nyingine ya matibabu.

Post a Comment
karibu kwa maoni