Kwa kawaida
chama kilichopo madarakani ndicho ambacho kinakuwa na kauli kwani hata ilani
inayotekelezwa huwa ni ya chama husika.
Hata
viongozi wanaoteuliwa hufuata misingi na nyayo zilizopo ili kuleta msisimko wa
Maendeleo katika Nyanja mbalimbali.
Mkuu wa mkoa
wa Manyara Alexender Pastory Mnyeti amekuwa akitoa kauli ambazo zimekuwa
zikiwakera wapinzani kwa namna moja ama nyingine.
Wakati akikaribishwa
rasmi kuanza kazi katika mkoa wa Manyara alisema kuwa wapinzani waliopo katika
mkoa huo watulie kwa kuwa ilani inayotekelezwa ni ya chama cha Mapinduzi.
Lakini pia
hivi karibuni akiwa katika ziara zake za kikazi katika wilaya zake alisikika
akisema
"Kwanza
niwatambue CHADEMA kama nani? Mimi si NEC wala msajili wa Vyama vya Siasa.
Pili
nishirikiane nao katika kutekeleza ilani ipi? Nimesoma ilani yote ya uchaguzi
ya CCM ya mwaka 2015 sijaona mahali pametajwa CHADEMA, sasa nalazimika vipi
kushirikiana nao?" ~ RC Mnyeti
Post a Comment
karibu kwa maoni