Uongozi
wa Waislamu Mkoani Rukwa umepokea kwa furaha mchango wa Shilingi
Milioni 5.7 uliotolewa na uongozi wa serikali ya Mkoa wa Rukwa
ukiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo katika kikao cha
maridhiano juu ya ujenzi wa msikiti uliosimama kwa muda.
Fedha
hizo zilizochangwa zilijumuisha ahadi, fedha taslimu pamoja na vifaa
vya ujenzi vilivyotolewa kwa umoja wa viongozi wa serikali kuonesha
mshikamano uliopo kati ya serikali na wananchi bila ya kujali itikadi,
dini wala rangi huku Wangabo akichangia milioni 1.5.
Kabla
ya maridhiano hayo Wangabo alitoa salamu za rais Dk. John Pombe
Magufuli juu ya kuuendeleza msikiti huo na kunukuu kuwa Mheshimiwa Rais
ametoa kibali cha kuuendeleza msikiti huo na yupo tayari kuweka jiwe la
msingi ama kuuzindua msikiti huo.
“Mh.
Rais ameniagiza niseme yafuatayo kuwa ametoa kibali cha kuendelea
kujenga msikiti huu hadi umalizike, ameyafikiria mambo mengi sana mpaka
kuja kufikia maamuzi haya, ili yalete mustakabali wa maridhiano, ilete
amani, ilete utulivu, mshikamano, maoelewano na umoja ili Rukwa yetu
iweze kusonga mbele kama kitu kimoja., la pili alisema kuwa yupo tayari
kuweka jiwe la msingi ama la kuzindua msikiti huu,”
Wangabo
aliuomba uongozi wa uislamu mkoa kuendelea kushirikiana na kudumiasha
amani na kuhakikisha wanajenga Rukwa moja isiyoyumbishwa na tofauti
yoyote kwani ushirikiano huo umekuwa wa muda mrefu hovyo asingependa
pawepo na tofauti.
Pia
alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha vikwazo
vyote vinaondolewa na kumtaka kamishna wa ardhi Nyanda za Juu Kusini
kufanya haraka kupitisha kibali ili msikiti huo upatiwe hati.
Kwa
upande wake Shekhe Mkuu wa mkoa wa Rukwa Rashid Akilimali amesifu
maamuzi ya rais Dk. John Pombe Magufuli na kukubali ombi lake la kutaka
kuja kuweka jiwe la msingi ama kuuzindua msikiti huo na kuwa waislamu
wataendelea kuungana naye na kumuombea amalize vipindi vyake salama.
“Mh.
Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya waislamu wa mkoa wa Rukwa kwanza tunatoa
shukrani za dhati kwa Mh.Rais wa nchi Mh. Dk. John Magufuli, nimeamini
kama alivyosema kuwa yeye ni msikivu na yeye anatuomba kila siku
tumuombee dua na sisi mwisho wa khotuba yetu kila ijumaa tunadua huwa
tunaiomba, Eee Mola wetu linda amani ya nchi yetu na uwalinde viongozi
wetu,” alisema Shekhe Akilimali.
Uongozi
wa mkoa wa Rukwa uliowajumuisha kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa,
Wakuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa halmashauri, Mbunge wa jimbo la
Sumbawanga mjini, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sumbawanga pamoja na kaimu
Kamishna wa Ardhi Nyanda za Juu Kusini.
Post a Comment
karibu kwa maoni