Chombo cha anga za juu cha China kilichoharibika kimeingia katika anga
la dunia asubuhi ya leo na kupasuka vipande vipande kikitarajiwa
kuanguka Kusini mwa Bahari ya Pasifiki. Kituo cha anga za juu cha China
kimesema kupitia mtandao wake, kwamba chombo hicho, Tiangong-1,
kimeingia katika anga la dunia saa 2 na dakika 15 saa ya China, na
kusisitiza kuwa hakitasababisha uharibufu wowote. Awali, wataalamu wa
masuala ya anga za juu walikuwa wamesema ingekuwa vigumu kujua chombo
hicho kingeanguka sehemu gani, hadi muda mfupi kabla ya kuingia katika
anga la dunia. Chombo cha Tiangong-1 kilipelekwa anga za juu mwaka 2011,
ikiwa hatua kubwa kwa China katika juhudi za kujenga kituo chake
binafsi cha anga za juu. Mwaka 2016 chombo hicho kiliharibika, na
wanaanga wamekuwa wakisubiri kurejea kwake duniani. China imekanusha
taarifa za vituo vya anga vya kigeni, kwamba imepoteza udhibiti wa
chombo hicho.
Home
»
Habari moto Kimataifa
»
Habari moto kitaifa
» CHOMBO CHA ANGA CHA CHINA CHAANGUKIA BAHARI YA PASIFIKI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
karibu kwa maoni