Katika kuboresha huduma ya afya na kuokoa vifo vya mama na mtoto vijijini, wahudumu wa afya wemapatiwa mafunzo maalumu ya siku ishirini na moja katika Tarafa ya Mbugwe yenye kata tano,vijiji ishirini na moja.
Vijiji hivyo ni vya mwada,Nkaiti,Vilima
Vitatu,Matufa,Mapea,Maghara pamoja na
vijiji vingine ambapo wahudumu hao wamepewa mafunzo ya kuokoa maisha ya mama na
mtoto katika vijiji vyao.
Mpango huo ni wa shirika la World Vision Tanzania
[ADP] ya Magugu kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wahudumu hao
wanapata mafunzo yaliyo bora ili kuokoa maisha ya wanachi.
Mratibu wa mradi huo kutoka World Vision ADP Magugu
Bwana Majdi Mfinanga amesema shirika litawasaidia kuwapatia vifaa vinavyohitajika
katika kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu zaidi ikiwemo baiskeli zitakazo
wasaidia kufika haraka katika eneo wanalo hitajika.
Naye kaimu mganga mkuu wa wilaya ya babati Madama
Hosea amewataka wahudumu hao kwenda kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa li kuepusha vifo vya mama
na mtoto.
Dr. Hosea ameahidi kuwa serikali itawapa
ushirikiano wa kutosha ikiwemo kuwatambua na kuwapa sitahiki zinazostahili na
kuwaomba wananchi kuwapa ushirikiano wa hali na mali kwani lengo la serikali ni
kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wote waishio Vijijini na Mijini.
Hata hivyo wahudumu hao wameahidi kufanya kazi
kwa ufanisi zaidi kwasababu wamepatiwa mafunzo mazuri ambayo yatawasaidia
kufanya kazi zao vizuri.
Post a Comment
karibu kwa maoni