0

 BABATI
Na
John Walter

Vijiji vitano vya wilaya ya Babati  mkoani  Manyara vinatarajia kunufaika namradi mkubwa wa maji utakaogharimu shilingi bilioni moja.
Akizungumza na kituo hiki mhandisi wa maji halmashauri ya wilaya ya Babati Onesmo Joachim amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo unategemea fedha kutoka serikali kuu.
Amesema kuwa utekelezaji wa mradi huu ulishaanza mapema mwaka huu ukasimama kwa muda kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hali iliyopelekea ziwa kujaa na kusababisha kushindwa kupitisha mabomba ambayo yanapitia pembezoni mwa ziwa hilo kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotumika katika nchi zilizoendelea.
Ameeleza kuwa  maji wanayachukua kutoka katika kijiji cha Moya maghara kupeleka maji katika vijiji vitano kupitia kando ya ziwa manyara ambapo  utavisaidia vijiji vitano ikiwemo minjingu,Kakoi,Olasiti,Vilima vitatu na Ngorei vinavyokabliwa na uhaba mkubwa wa maji.
Mradi huo unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Amewataka wanakijiji hao waendelee kutoa mchango wao ili kufanikisha zoezi hilo ambalo limelenga kuwatoa katika adha ya maji wanayokabiliana nayo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top