0
Mwanamke mmoja Zuhura Hamisi ambaye alikuwa na uja uzito wa miezi miwili kata ya Magugu kijiji cha Matufa wilayani Babati Mkoani Manyara amecharangwa mapanga na mwanaume aliyekuwa akiishi nae Ramadhani Shabani kisha kutoa kichanga hicho tumboni na kumhifadhi ndani ya mfuko wa Salfeti uliokuwa na viungo vya mwili wa mama yake na kutokomea kusikojulikana.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu alieleza kuwa awali marehemu alikuwa akijulisha na kazi katika Hoteli huko Magugu ndipo mwanaume huyo akamwambia kuwa wakaishi pamoja kama mume na mke.
Walienedelea kusema kuwa baada ya marehemu kufika nyumbani na kumkuta na mwanamke mwingine ndipo ugomvi ukazuka na kusababisha mauaji hayo ya kinyama.
Walisema kwamba mwanaume huyo hakuwahi kumtambulisha nyumbani kwao na alipomtaka afike kwao ili atambulike na wazazi alidai kuwa ipo siku wataenda wala asijali.
Kinachoonekana ni kwamba mwanaume huyo alimuwekea madawa ya kulevya kwenye soda aliyomletea mwanamke wake siku hiyo baada ya ugomvi bila yeye kutambua hali iliyomsababishia usingizi mzito kisha kuchukua sime na kuanza kumkata kiungo baada ya kiungo.
Majirani wanasema kuwa walihisi harufu mbaya iliyokuwa ikitokea katika nyumba hiyo ndipo walpofika na kukuta inzi wakiwa wametanda huku mlango ukiwa umefungwa kwa nje na kuamua kuuvunja mlango.
Walisema kuwa Ramadhani alimkuta Zuhura akiwa na watoto wawili,siku ya tukio hilo mwanaume huyo aliwapeleka kwa rafiki yake anaeishi karibu nae na alipokuja mama kuwaulizia aliwaelekeza walipo ndipo mama kufika na kuwakuta tayari wameshalala akaamua kuwaacha ili kesho yake akawachukue lakini hakujua kitakachofuata baadae.
watoto walikuwa kwa jirani .
Mwandishi wa habari hii anatoa rai kwa wananchi kutoa taarifa mapema pindi wanapoona matukio ya uhalifu na ukatili kama hayo katika vyombo husika wakiwemo viongozi wa mitaa au vijiji.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amin.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top