0

Kata ya Selela Monduli Mkoani Arusha inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa umeme kwa zidi ya wiki nne sasa na kusababisha shughuli nyingi kukwama ikiwemo hospitali ya zahanati katika kata hiyo kushindwa kutoa huduma kwa wagonjwa  ipasavyo hali  iliyowakasirisha  wakazi wa Kata na kijiji cha Selela na kumtaka diwani wao ashuhulikie hilo mara moja.
Kata ya selela jimbo la Monduli inakabiliwa na tatizo la umeme zaidi ya mwezi sasa.
Diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi [CCM]  Mh.Casbeth Meena amezungumza na kipindi hiki na kueleza kuwa amewasiliana na Tanesco makao makuu jijini Arusha na mpaka sasa hakuna dalili zozote za kutatuliwa kwa tatizo hilo na kueleza kuwa watalishtaki shirika la umeme kwa kuwakosesha wananchi wa Kata na kijiji cha Selela huduma hiyo huku wakiwa tayari wameshalipia.
Diwani Meena amesema kwamba amepanga kulishtaki shirika la umeme [TANESCO] endapo watashindwa kulitatua tatizo hilo mapema.cue Diwani
Diwani huyo amesema kuwa tangu Transfoma iliyokuwa imefungwa kwenye kata hiyo  iungue mpaka leo hakuna kilichoendelea.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa ramani ya kijiji inaonyesha kuwa kijiji kizima kingepata umeme pamoja na shule ya ya Sekondari lakini shule hiyo ya Kata haina umeme na wanafunzi wanatumia  sola kusomea.
Kipindi cha nyuma shule ya kata hiyo ilikuwa ikitumia taa katika kujisomea.
Meena anaeleza kuwa kwa kukosekana kwa umeme unasababisha shuguli nyingi za kijamii kukwama kama vile mashine za kusaga,wanaojishughulisha na kuchomelea [welding] Saloon na kushindikana kufanyika kwa vipimo muhimu katika zahanati ya kata.
Amesema kuwa atawasiliana na waziri mwenye dhamana wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ili amweleze malalamiko hayo yaliyopo katika kata yake.

kuipata sauti ya diwani bonyeza hapa. http://www.audiomack.com/song/stove-iron/casbeth-meena

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top