0
Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowassa amesema kuwa michango  bado inahitajika kwa wahanga wa Tetemeko LA ardhi Mkoani Kagera.

Bw:Lowassa amemueleza hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera baada ya kuwa ametembelea katika Kara za Hamugembe pamoja na Kashai Manispaa ya Bukoba na kujionea Namba watu na Majengo walivyo athirika kutokana na tetemeko LA ardhi lililotokea septemba 10 Mwaka huu.

Amesema kuwa baada ya kujionea madhara hayo ambapo makazi ya Wananchi hao yameathiriwa vibaya amechangia Mifuko Mianne (400) ya Simenti huku akimuomba  Mkuu wa Mkoa huo wa Kagera Kutafuta wataalamu wa Video kutengeneza Makala zitakazo rushwa ili kuwa wezesha Wadau Mbalimbali wa Maendeleo kujionea hali ambayo tetemeko hilo lilivokuwa hususan kwa wale ambayo hawakufanikiwa kufika Mkoani Kagera.

Hata hvyo amesema kuwa Mchango wake huo wa mifuko hyo 400 Inakadiliwa kuwa na  thamani ya Shilingi Milioni Saba(7) ambayo amesema kuwa itakabidhiwa kwa Meya wa Manispaa hiyo ya Bukoba.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top