0
WatuWatatu Wamehukumiwa Kifungo cha Maisha Jera Mkoani Kagera Baada ya kukutwa na hatia ya Kuchoma Makanisa Mkoani humo. 

Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mjini Bukoba  na Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Namba 178 na Namba 67 Victor Bigambo amewakuta na hatia baada ya kusikiliza pande zote husika na kujiridhisha na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo.

Akizungumza na Waandishi wa habari Nje ya Mahakama hiyo Mjini Bukoba Naendesha Mashitaka Mayele Emmanuelly amesema kuwa washitakiwa hao katika kesi Namba 178  pamoja na 67 wamehukumiwa Maisha huku katika shauri la  kula njama katika kesi hiyo Namba 67 wamehukumiwa Miaka Saba.

Amewataja washitakiwa hao kuwa ni pamoja na Ngesele Joseph, Rashid Mzee na Mwingine aliyetambuliwa kwa Majina ya Aguli Dauda , amesema kuwa Nje na mashauri hayo wawili lakini pia kuna mashauri zaidi ya 16 ya uchomaji wa Makanisa Mkoani humo na pamoja na mengine kati ya hayo ya Mauwaji.

Nae Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera Augustine Olomi amesema kuwa Wananchi waendelee kutoka TAARIFA  kwa Kesho hilo ili kuwabaini watu wengine waliohusika na Vitendo hivo na kwamba wao kama Walinzi wa amani watahakikisaha Wananchi Wanalindwa na Mali zao.
             

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top