0
HALMASHAURI ya Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanajaro, imeanzisha kampeni maalumu ya kuwasaka na kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wanaoshirikiana na watoto wao wa kike kuwaficha wanaume wanaowapa ujauzito.
Tayari mwanamke na binti yake, wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kushirikiana kutoa mimba ya msichana huyo.
Mwanamume aliyempa ujauzito anaendelea kusakwa ndani na nje ya wilaya hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Magreth John, amesema hayo wakati akizungumzia mipango ya halmashauri kukabiliana na vitendo vya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kukatishwa masomo kwa kupewa ujauzito.
Amesema kampeni hiyo endelevu, inafuatia wanafunzi 60 wa shule za msingi na sekondari kupewa ujauzito kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu, wilayani humo.
John amesema wapo baadhi ya wazazi na walezi hushirikiana na binti zao, kuwaficha watuhumiwa wanaowapa mimba, jambo ambalo halikubaliki na linarudisha nyuma kiwango cha taaluma wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadiki amesema, serikali imelazimika kuagiza idara ya afya kuwapima wanafunzi wote kuanzia shule za msingi na sekondari iwapo wana mimba mara wanapofunga au kufungua shule.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top