0
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (kulia) akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Umoja huo, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Wajumbe walioshiriki mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) anayeshughulikia masuala ya Nchi Masikini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (wa pili kulia), ambapo masuala kadhaa yakiwemo maendeleo ya Sekta Binafsi na Miundombinu yalijadiliwa kwa kina wakati ujumbe huo kutoka UN ulipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Ofisini kwake Jijini Dar es salaam.
Wajumbe walioambatana na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) alipokuwa akielezea umuhimu wa amani katika maendeleo ya Bara la Afrika, wakati wa kikao chake na Kiongozi huyo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.



Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya  Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (kulia) akisikiliza kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani), alipokuwa akielezea miradi itakayowakwamua wananchi kiuchumi ikiwemo ile ya Kilimo itakayosaidia kuendesha viwanda. Mazungumzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kushoto), akifurahia jambo wakati Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya  Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (hayupo pichani), akielezea ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa, wakati wa kikao kilichofanyika Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top