Home
»
Habari moto kitaifa
» Maji yawa kero kwa wanakijiji wa King'ori......yazuiwa na kijiji jirani..Viongozi wakwama.
Wanakijiji
wa kijiji cha King'ori Arumeru mkoani Arusha wanalazimika kununua maji
shilingi 600-1000 kwa ujazo wa lita ishirini kwa kutokana na kukatiwa
maji na kijiji jirani cha Ngwasenga huku wakiwatishia kuwadhuru endapo
watajaribu kwenda katika kijiji hicho kwa dhumuni la kutaka maji.
Kwa
mujibu wa taarifa za uhakika kutoka katika kijiji hicho Viongozi
mbalimbali wameshafuatilia na jitihada zao zote zimekwama wakielezwa
kwamba hata wamfikishie taarifa hizo rais John Magufuli hawataruhusu
maji kwenda King'ori.
Kwa sasa maji wanayapata kupitia visima vya asili tena katika umbali mrefu na kutembezewa kwa Maboza kwa gharama kubwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni