Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi mbalimbali za umma zinazodaiwa
na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ziwe zimelipa madeni yao ifikapo Juni
30, mwaka huu.
TTCL
inazidai taasisi mbalimbali za umma jumla ya sh. bilioni 11.5 ikiwa ni
gharama ya huduma walizozitoa kwa taasisi hizo, hivyo kukwamisha
utendaji wa kampuni hiyo.
Ametoa
agizo hilo jana (Ijumaa, 10 Februari, 2017) wakati akizindua huduma za
simu ya mkononi kwa teknolojia ya 4G LTE ya TTCL mjini Dodoma.
Pia
amemtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa akutane na wadaiwa sugu wote wathibitishe madeni husika na
kisha wapange namna ya kulipa.
“Nijuavyo,
kila Wizara inatenga bajeti kwa ajili ya ankara za simu, sasa haya
malimbikizo yanatoka wapi?. Ni lazima wadaiwa wote walipe madeni yao
mara moja,” aliagiza.
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa “unapokuwa na deni lazima ulipe. Mheshimiwa Waziri
simamia hili, na unipe taarifa ya utekelezaji kabla ya Mkutano ujao wa
Bunge la Bajeti,”.
Pia
Waziri Mkuu alitoa rai kwa Menejimenti na watumishi wa TTCL kwa
kuwataka watambue dhamana waliyopewa na waitendee haki kwa kufanya kazi
kwa bidii na weledi.
“Fanyeni
kazi kwa bidii, weledi, uzalendo, maarifa na ubunifu wa hali ya juu.
Imarisheni Idara ya Masoko, hamasisheni ubunifu kwenye Kampuni na wapeni
nafasi vijana wenye uwezo,”.
“Kama
hiki ni kizazi cha T, wacha kizazi hicho kiongoze mapinduzi ya T,
muhimu uzalendo, uwezo, dhamira na ubunifu vizingatiwe katika kutoa
nafasi hizo,”. alisisitiza.
Pia
aliwataka viongozi wa TTCL wapitie upya muundo wake na wajiridhishe
kama unaendana na ushindani wa kibiashara na dhamira ya Serikali ya
kupunguza gharama zisizo za lazima.
Akizungumzia
suala la idadi ya watumishi wa Kampuni, Waziri Mkuu ameshauri
wajifanyie tathmini wenyewe kujua mahitaji halisi ya watumishi na
kufanya maamuzi kwa kuzingatia sheria za nchi.
“Serikali
inatarajia TTCL ijiendeshe kwa faida na sio kuja kuiomba Serikali
ruzuku, hivyo hamna budi kupunguza gharama za uendeshaji wa kampuni kwa
kadiri inavyowezekana,” alisema.
Awali,
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba alisema miongoni
mwa changamoto zinazokabili kampuni hiyo ni pamoja na mtaji mdogo.
Pia
aliiomba Serikali iwasaidie ili waweze kulipwa madeni yao wanayozidai
taasisi mbalimbali za umma kutokana na huduma walizozitoa kwa taasisi
hizo.
Hata
hivyo Bw. Kindamba ameahidi kwamba watafanya kazi kwa biidi ili
kuhakikisha TTCL inaongoza kwa kutoa huduma bora za mawasiliano nchini.
Post a Comment
karibu kwa maoni