0


Image result for gekul babati 
Hali ya mbunge wa Babati mjini Paulina Gekul [CHADEMA]inaendelea kuimarika baada ya kupata ajali ya gari akiwa kwenye ziara ya naibu waziri wa Muungano na Mazingira Luhaga Mpina.
Ajali hiyo ilitokea jumamosi ya wiki iliyopita [24.2.2017] baada ya gari la mbunge lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka katika mtaa wa Nangara ziwani mjini Babati bara bara ya kuelekea Dodoma.
Mbunge huyo alijeruhiwa  kichwani. 
Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati mjini alikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U na baadaye taarifa ilizozipata blog hii ni kwamba alihamishiwa katika hospitali ya KCMC Moshi kwa uchunguzi zaidi. 
Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira alilazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.
Naibu waziri alikuwa katika ziara yake ya kikazi kwa siku mbili katika mji wa Babati akitembelea maeneo mbalimbali,alikitembelea kiwanda cha Perfume SIERA,Eneo la Dampo Sigino,Ziwa Babati na kujionea gari la taka la kisasa lililonunuliwa kwa pesa za Halmashauri lenye thamani ya shilingi milioni 230.


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top