0
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson asema Marekani imechoka kuivumilia Korea Kaskazini
Image captionWaziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson asema Marekani imechoka kuivumilia Korea Kaskazini
Sera ya Marekani ya kuwa na subra dhidi ya Korea Kaskazini imeisha, kulingana waziri wa maswala ya nje nchini humo Rex Tillerson wakati wa ziara yake nchini Korea Kusini.
''Njia zote tulizotumia ziko wazi na sasa tunatafuta njia nyengine za kidiplomasia ,usalama na kiuchumi'' ,alisema.
Korea Kaskazini imezua wasiwasi kufuatia hatua yake ya hivi karibuni kufanyia majaribio makombora na silha za kinyuklia.
Bwana Tillerson alizungumza muda mfupi baada ya kuzuru eneo lisilo na wanajeshi linalozigawanya nchi hizo mbili za Korea.
Amesema kuwa juhudi za miaka 20 za kuibembeleza Korea Kaskazini kuwacha mipango yake ya kinyuklia zimegonga mwamba.
Alipoulizwa iwapo kuna uwezekano wa kuichukulia hatua za kijeshi alisema: Hatutaki kuchukua hatua kama hizo lakini akaongezea kuwa iwapo wataendeleza vitisho vyao hadi kufikia kiwango ambacho kinahitaji kuchukuliwa hatua basi hakutakuwa na chaguo jingine.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top