0
Bw Felix Kaweesi akihutubia wanahabari mjini Kasese 30 Novemba, 2016Haki miliki ya pichaAFP
Image captionBw Felix Kaweesi akihutubia wanahabari mjini Kasese Novemba mwaka jana
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Felix Kaweesi amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana.
Taarifa zinasema Bw Kaweesi ameuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa anaondoka kwake nyumbani Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.
Walinzi wake wawili walioandamana naye pia wameuawa.
Bw Kaweesi aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana.
Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake. Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.
Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mulago.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top