0
wqq

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuandaa siku ya mazoezi ya hiari kila ifikapo jumamosi ya pili kila mwezi ili kuepuka magonjwa yasioambukiza.

Samia aliagiza hivyo ili kuwajengea wananchi kuwa na mazoea ya kufanya mazoezi ili kuweka jitihada za kujikinga magonjwa mbalimbali.

“Watanzania tupende kufanya mazoezi mara kwa mara ili tuweze kuepuka magonjwa yasioambukiza yakiwemo Kisukari, magonjwa ya moyo, saratani ambayo yanasababishwa na mafuta mengi mwilini ”alisema Mhe. Suluhu.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk. Joel Bendera alisisitiza hilo kwa wakazi wa mkoa wa Manyara huku viongozi wengine wakilipigilia msumari na kufanywa kwa vitendo kila jumamosi.

Asubuhi ya leo wananchi wakiwa na baadhi ya viongozi wa serikali walikimbia kutoka uwanja wa kwaraa mjini Babati mpaka kona ya kuelekea Sigino wakiongozwa na Dulla wa Dom kiongozi wa Jogging Babati.

Kampeni hii ya kufanya mazoezi imeandaliwa na Wizara ya Afya  imezinduliwa rasmi Desemba 17 2016 ikiwa na lengo la kupambana na magonjwa yasioambukiza kama vile kisukari, Shinikizo la Damu, uzito uliozidi kiasi , utapia mlo na magonjwa ya moyo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top