Kamati ya saa 72 hatimaye imefanya maamuzi yake kuhusu Rufaa ya klabu ya Simba iliyoiwasilisha katika kamati hiyo Dhidi ya Klabu ya Kagera Sugar kumchezesha mchezaji wao mwenye kadi 3 za njano
Maamuzi hayo yametangazwa usiku wa leo na mwenyekiti wa Bodi ya Ligi na kusema ni kweli wamejiridhisha kuwa timu hiyo ilimchezesha mchezaji huyo ili hali wanajua ni kinyume na sheria, na adhabu yake ni timu hiyo kunyang'anywa ushindi, na kupewa timu pinzani, na ndicho walichkifanya
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ahmed Yahya amewaambia Waandishi wa Habari usiku huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kwamba Kamati ilibaini ni kweli Kagera Sugar walifanya kosa hilo la kikanuni na adhabu yake ni kupokonywa ushindi.

Post a Comment
karibu kwa maoni