0
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imebainisha kuwa gharama halisi za kumtunza Faru mzee kuliko wote katika hifadhi hiyo mwenye umri wa miaka 54. faru fausta zilizotumika kuanzia mwezi septemba 2016 mpaka sasa ni shilingi milioni kumi laki moja na tisini na tisa na si shilingi milioni 64 kama zinavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Naibu mhifadhi anaeshughulikia uhifadhi maendeleo ya jamii na utalii Dr. Maurusi Msuha amebainisha kuwa gharama halisi za kumtunza faru fausta kwenye banda hilo zikihusisha matibabu, chakula na ulinzi kwa mwezi ni shilingi milioni moja laki nne na arobaini na tano.
Baada ya kuwa chini ya uangalizi maalum kwa miezi kumi huku akipatiwa matibabu chakula na ulinzi Afya ya Faru Fausta anayeishi katika banda ndani ya bonde la Ngorongoro imeimarika na hii ni kwa mujibu wa daktari Kuya Sayalal anaye muhudumia mnyama huyo kwa ukaribu.
Hatua ya kumpa uangalizi maalum faru fausta ilikuja Baada ya uongozi wa mamlaka kubaini kuwa faru huyo alikuwa akiandamwa na magonjwa na wakati mwingine kuliwa na fisi na kusababishia vidonda na zaidi kushindwa kujitegemea katika shughuli za kawaida za kujitafutia malisho hali iliyotokana na uzee na uoni hafifu mamlaka ya ngorongoro iliona ni busara kumtunza faru huyo katika banda maalum lililojengwa kwa lengo la kuweka wanyama waliokuwa na matatizo ya kiafya ili wapate uangalizi wa karibu shabaha ikiwa ni kuhakikisha wanaendelea kuishi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top