0
Image result for roma mkatoliki
Taarifa za kupotea kwa Msanii Roma Mkatoliki na wenzake watatu baada ya kutekwa na kuchukuliwa na Watu wasiojulikana kwenye studio za TONGWE Dar es Salaam, zilianza kusambaa kuanzia juzi usiku (April 5 2017).
Leo April 7 2017 Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambayo iko chini ya Dr. Mwakyembe imetoa taarifa ifuatayo  “Kwa dhamana yake katika tasnia ya Sanaa, Wizara imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma Mkatoliki””.
Wizara imefuatilia kwa karibu suala hili kwa kuwa lina muelekeo wa jinai. Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi.
Kutokana na hali hiyo, Wizara inawaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.
Related image
Msanii Moni anayedaiwa kutekwa yeye pamoja na Roma na wengine wawili.
Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema ni wakati wa kuwa watulivu.'Tunapopotelewa na watu wetu katika mazingira ambayo hatuyafahamu sio wakati wa kurusha rusha maneno na kufikia hatua ya kupotza ushahidi,kama huna taarfa sahihI usiandike chochote."
"Nikiwa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzoi na usalama ya mkoa niwahakikishie haitafika jumapili tutakuwa tumewapata ndugu zetu wote wanne.Tuwaombee ndugu zetu".
Waliowakamata sio askari polisi ni watu waliofika na virungu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top