0
1.Simon Msuva. Mcheza soka katika timu ya taifa Taifa Stars na pia winga wa klabu ya Yanga Simon Msuva anaongoza orodha hii, Msuva hadi sasa ana followers 207,000 na ndio mchezaji anayeongoza akiwa amewaacha wenzake kwa mbali sana.
2.Juma Kaseja. Golikipa wa Kagera Sugar ambaye pia amepitia vilabu vya Yanga na Simba Juma Kaseja yuko nafasi ya pili akiwa na idadi ya followers 115,000 katika ukurasa wake wa Instagram.
3.Haruna Nyionzima. Wakati Msuva anaongoza kwa idadi ya followers instagram anayemfuatia kwa idadi kubwa ya followers kutoka Yanga ni Haruna Nyionzima, Mnyarwanda huyo hadi sasa ana idadi ya followers 114,000 katika ukurasa wake wa Instagram.
4.Deus Kaseke. Yanga tena wanakuja katika nafasi ya nne hii inamaanisha nne bora ni mchezaji mmoja tu asiyetokea Yanga, Kaseke yupo katika nafasi hii akiwa na followers 109,000 katika ukurasa wake wa Instagram.
5.Paul Nonga. Mshambuliaji wa Mwadui Fc anatokea katika nafasi ya tano, huyu ni Nonga ambapo Nonga ana followers 101,000 katika ukurasa wake wa Instagram
6.Juma Abdul. Nafasi ya 6 pia ni Yanga, Juma Abdul yuko katika nafasi hii kwa kuwa na followers 96,800 katika ukurasa wake huo wa Instagram.
7.Mohamed Hussein. Nafasi ya saba ndio kumetokea mchezaji wa kwanza ambaye ni Simba na ni beki wa Simba Mohameid Hussein Tshabalala ambaye ana idadi ya followers 96,200 katika ukurasa wake wa Instagram.
8.Said Ndemla.Kiungo wa Simba Saidi Hamisi Ndemla yuko katika nafasi ya 8 akiwa ana followers 81,900 ikiwa ni pungufu ya followers 14,300 kutoka alipo Tshbalala.
9..Mrisho Ngassa. Nafasi ya tisa inashikiliwa na winga wa zamani wa klabu ya Yanga ambaye kwa sasa anakipiga Mbeya City Mrisho Ngassa. Ngassa anao followers 88,700 katika mtandao wake wa Instagram.
10.Himid Mao. Nafasi ya 10 ni kiungo mkabaji wa Azam Fc Himid Mao “Ninja”, Himid ameingia katika kumi bora ya wasakata kabumbu wa Tanzania wenye followers wengi akiwa na followers 74,400.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top