Matukio
ya watu kuchukua maamuzi ya kujiua katika manispaa ya Shinyanga
yanazidi kushika kasi ambapo jana Jumapili June 18,2017 majira ya saa
10 alfajiri kijana aitwaye Paulo Ezekiel (17) mkazi wa mtaa wa Mazinge
kata ya Ndembezi alifariki dunia kwa kujinyonga kwa kamba juu ya mti
jirani na nyumba yao.
Inaelezwa
kuwa huenda ni ugumu wa maisha ndiyo umechangia kifo cha kijana huyo
kwani enzi za uhai wake alikuwa analalamika kuwa maisha ni magumu.
Baba
mzazi wa marehemu Ezekiel Paulo anasema majira ya saa 10 alisikia
mlango wa chumba cha kijana wake ukifunguliwa akadhani pengine ametoka
kwenda kujisaidia lakini hakurudi tena ndipo alipoingiwa na wasiwasi na
kuanza kumsaka.
“Tuliamshana
tukaanza kumsaka kila mahali baadaye tukamuona akiwa juu ya mti jirani
na nyumba yetu tayari amefariki dunia”, ameeleza Paulo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Jumanne Murilo amethibitisha kutokea kwa tukio.
Matukio
ya watu kuchukua uamuzi wa kujiua yameanza kukithiri katika manispaa ya
Shinyanga ambapo ndani ya mwezi mmoja huu wa Juni hili ni tukio la nne.
Tukio
la kwanza ni la Luhende Lusangija (34) mkazi wa kata ya Ngokolo
aliyejiua kwa kamba,la pili ni la Mwenyekiti wa waendesha bodaboda
katika manispaa ya Shinyanga Jacob Paul mkazi wa kata ya Ngokolo
aliyejiua kwa waya wa simu la tatu ni la Saada Elias mkazi wa kata ya
Ndembezi aliyekatisha maisha yake kwa kujichinja kwa kisu na chupa ya
soda.
Post a Comment
karibu kwa maoni