Kanisa moja katika mji mkuu wa
Ghana, Accra, limeandaa ibada ya kutoa shukrani kutokana na ufanisi wa hivi
majuzi wa Chelsea katika Ligi ya Premia.
Mchungaji Azigiza ambaye ni shabiki
damu wa klabu hiyo aliwahamisha waumini wafike kwa ibada wakiwa wamevalia
fulana za klabu hiyo.
Alisimama juu ya keki ya Chelsea
kwenye jukwaa ambalo lilikuwa limejengwa kufanana na uwanja wa soka.
Alisema: "Chelsea, kwa kudura
zake Mungu, walimaliza wa kwanza."
Aliambia BBC kwamba alitaka kutumia
nguvu za soka kuzungumzia kuhusu Mungu.
Azigiza pia aliongoza waumini kuimba
aya ya wimbo wa klabu ya Chelsea, Blue is the Colour.
Pasta huyo, ambaye wakati mmoja alikuwa
DJ wa redioni, alikuwa pia anamtania mkuu wake katika kanisa hilo la Living
Streams International Church, Pasta Ebenezer Markwei, ambaye ni shabiki wa
Arsenal, na ambaye alikuwa amemkaribisha kwa ibada hiyo
Haki miliki ya picha Living Streams
International Image caption MKuu wa awali wa Pasta Azigiza, Ebenezer Markwei
(kulia) ni shabiki wa Arsenal
Pasta Markwei alitoa mahubiri kuhusu
"mema, mabaya na maovu ya ushindani" akidokeza kwamba mashabiki wa
soka wanafaa kushiriki katika ushindani mwema.
Alisema kuna mambo mema sana katika
kfuurahia ufanisi wa watu wengine.
Post a Comment
karibu kwa maoni