HALILA
TONGOLANGA, mwanamuziki wa siku nyingi ambaye alikuwa amelazwa katika
hospitali ya Muhimbili amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Halila
alikuwa amesafirishwa kutokea Ndanda kuja Muhimbili akihisiwa kuwa na
matatizo ya figo. Licha ya kuwa alifika Muhimbili juzi Ijumaa usiku,
lakini alikuwa hakufanyiwa vipimo vyovyote vikubwa mpaka umauti
unamkuta.
Jana
Jumapili ililazimika kuanza kufanya jitihada za kupata daktari ambaye
angemshughulikia kwa karibu zaidi, na daktari alipatikana ambaye
aliahidi angeanza kufwatilia swala lake leo asubuhi lakini mapenzi ya
Mungu yalikuwa tofauti.
Juzi nilipomuona alinambia kuwa ana mengi
anataka kunambia, lakini moja aliloweza kunambia pale ni kuwa yeye
anajihisi ana kansa, 'Nilimuuliza anajuaje hilo, kwa vile hajapimwa
hakuwa na jibu"
Wengi tutamkumbuka Tongolanga kwa wimbo wake wa Kimakonde aliouimba kwa mara ya kwanza akiwa na Les Mwenge 'Kila Munu Ave Na Kwao"
Mwili wa marehemu unategemewa kusafirishwa leo saa tano kuelekea kwao Newala. Habari zaidi zitawafikia kupia hapa
Mungu amlaze Pema peponi Halila Tongolanga

Post a Comment
karibu kwa maoni