0
Kada maarufu wa CHADEMA Mwanza ambaye pia aliwahi kugombea Ubunge Jimbo la Sengerema Hamis Tabasamu amerudisha kadi ya chama hicho na kujiunga rasmi CCM mbele ya Rais Magufuli.
Tabasamu ameomba radhi kwa uwongo aliokuwa akisema kuhusu Serikali wakati yupo CHADEMA huku akisisitiza kuwa amerudi CCM kutokana na kuvutiwa na utendaji wa Rais Magufuli baada ya kushughulikia masuala mbalimbali ikiwemo issue ya madini na kuzuia kitu ambacho aliwahi kukipigia kelele.
Rais Magufuli amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mwanza iliyoanza jana.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top