0
Timu hiyo ilikuwa imetoka kushiriki mchezo wa ligi kuuTaarifa kutoka Ghana zinasema kwamba pametokea ajali ya gari lililokuwa limebeba miongoni mwa timu kongwe nchini humo Asante Kotoko.
Mlezi wa timu hiyo ni mfalme wa Ashanti.Asante Kotoko ni miongoni mwa klabu zinazotoa upinzani mkubwa Afrika
Timu hiyo ilikuwa inarejea katika mji wake ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo , Kumasi baada ya mchezo wa ligi kuu mjini Accra dhidi ya Inter Allies FC.
Ajali hiyo imetokea katika sehemu iitwayo Nkawkaw kilomita 150 kutoka mji mkuu wa Ghana, Accra.
Inasemekana kuwa baadhi ya wachezaji wameumia vibaya akiwemo pia kocha wa timu hiyo na pia kuna kifo cha mtu mmoja.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top