0


Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa amewasili kwenye Wilaya ya Chato Geita akiwa ameambatana na mke wake Mama Anna Mkapa na kupokelewa na mwenyeji Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli.

Mzee Mkapa Jumatatu ya Julai 10 anatarajiwa kukabidhi nyumba kumi kwa hospitali ya Wilaya ya Chato zilizojengwa kwa ufadhili wa Mkapa Foundation.

Kwenye huo msafara, mstaafu Mkapa ameambatana na Balozi wa Japan hapa Tanzania Masaharn Yoshida ambaye Jumatatu hiyohiyo ya July 10,2017 atakabidhi mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti kwa chama cha ushirika wa kilimo na masoko Chato – AMCOSS

Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa anatarajiwa pia kuhudhuria mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na Mwenyeji wake Dkt John Pombe Magufuli siku hiyohiyo ya Jumatatu Julai 10,2017 kwenye uwanja wa Mazaina Chato mjini.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top