Tasnia
ya habari nchini imepata pigo kwa kumpoteza mtangazaji maarufu wa kituo
cha redio cha E-FM, Seth Katende maarufu kama ‘Bikira wa kisukuma’
aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kituo hicho cha redio kimeeleza kuwa Katende alipoteza maisha baada ya kuugua kwa muda mfupi.
“Kwa
masikitiko makubwa E FM inapenda kuwajulisha kuwa mwenzetu Seth Katende
maarufu” Bikira wa kisukuma”amefariki dunia katika hospitali ya Taifa
ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.Seth atakumbukwa sana kwa
ucheshi wake kupitia kipindi cha Ubaoni alichokua akiendesha sambamba na
Imma Kapanga na Mpoki au “mwarabu wa Dubai”.Msiba upo nyumbani kwa baba
yake mzazi Changanyikeni Dar es salaam,” ilieleza taarifa ya E-FM.
Katende
alianza kupata umaarufu kupitia mtandao wa Instagram akitumia jina la
‘Bikira wa Kisukuma’ akichambua mada mbalimbali za maisha zilizowagusa
wengi hususan vijana.
Umaarufu
wa marehemu uliongezeka mara dufu baada ya kuanza kusikika kupitia
kipindi cha Ubaoni cha E-FM kutokana na ucheshi wake na jinsi alivyokuwa
akiwasilisha mada mbalimbali.
Mungu ailaze roho yta marehemu mahali pema peponi amen .
Post a Comment
karibu kwa maoni