Mkurugenzi wa TCRA,
Mhandisi James Kilaba aliyasema jana Ijumaa kuwa, mamlaka hiyo imepokea
malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa simu wakilalamikia matangazo
hayo yanayotolewa na kampuni za simu.
Amesema tayari TCRA imeshaziandikia barua kampuni zote za simu kusitisha matangazo hayo na itakutana nazo kwa majadiliano ya kina Julai 6.
Amesema mamlaka haitambui utaratibu huo na inauchukulia kama kero kwa watumiaji wa simu ambao hutegemea kutumia njia hiyo ya mawasiliano kurahisisha mambo.
Katika siku za karibuni imekuwa ni kawaida kwa mtu anayepiga simu kusikiliza wimbo au matangazo ya biashara na baadaye kuambiwa namba anayopiga haipatikani.

“Tuna imani mtu anapopiga simu ana shida ya haraka na anahitaji
afanye mawasiliano, unapomuwekea matangazo kwa dakika tatu au nne ni
usumbufu,” amesema.
Katika siku za karibuni imekuwa ni kawaida kwa mtu anayepiga simu kusikiliza wimbo au matangazo ya biashara na baadaye kuambiwa namba anayopiga haipatikani.
Post a Comment
karibu kwa maoni