
Tume hiyo imesema matokeo ya awali
yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa.
Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu
muhula wa tatu wa miaka saba.
Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa
kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari
ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa.
Wapinzani wa bwana Kagame walikuwa
ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana
Rais Kagame aliingia madarakani
mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na
kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo
wa wastani waliuawa.
Katiba ya Rwanda ilifanyiwa
mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka
2034.
Wapinzani wa Kagame wamelalamika
kuwa wafuasi wao wanahangaishwa, wakisema kuwa ndiyo imesababisha kuwepo watu
wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura.
Hata hivyo chama tawala kimekana
madai hayo.
![]() |
Kutoka kushoto Paul Kagame, Frank Habineza na
Philippe Mpayimana
|
Post a Comment
karibu kwa maoni