Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia imetangaza ajira za walimu wa shule za msingi kwa walimu
ambao wamemaliza masomo yao mwaka 2014/2015 katika ngazi ya cheti (III
A).
Taarifa
iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia na kuthibitishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbas imesema kuwa walimu ambao wamemaliza mwaka 2014/2015 na walituma
maombi yao kwenye tangazo la kazi ya Agust 10, 2017 hawatakiwa kuomba
upya kwani barua zao zinafanyiwa kazi.
Post a Comment
karibu kwa maoni