0
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Aspire Media inayomiliki kituo cha Redio cha Sun rise Fm amesema ili kuhakikisha wanawapatia watanzania kile wanachokihitaji wameandaa program maalum kwa ajili ya waandishi wa habari wa Sun rise Fm.

Amesema hayo wakati wakizindua masafa yao mapya mkoani Manyara katika wilaya ya Babati ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara Dk. Joel Nkaya Bendera.

Akijibu swali aliloulizwa na WALTER HABARI kuhusu watu wanaotumia vibaya jina la mwandishi wa habari maarufu kama Kanjanja,Dionis Moyo amesema hilo wanalidhibiti na kwamba waandishi wake wana elimu ya kutosha kuanzia Diploma na kuendelea.

Malengo yetu ni kuhakikisha mwandishi/mtangazaji wa Sun rise redio elimu ya chini kabisa iwe ni Diploma.,,Alisema Moyo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top