Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Kanda maalum jijini Dar es salaam
Lazaro Mambosasa, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo
katika eneo la Kivule Chanika, ambapo polisi ilimjeruhi Annae Rashidi
Kapela maarufu kwa jina la Abuu Mariam alipokuwa akijaribu kukimbia, na
kufariki dunia akiwa njiani wakimpeleka hospitali.
"Askari walipojaribu kumsimamisha aligeuka na kuanza kukimbia, askari
walifyatua risasi na kumpiga kwenye goti, alipokamatwa jambazi huyo
alitaja mlolongo wa matukio yaliyowahi kuyatekeleza, jambazi huyo
amekiri kushiriki kwenye tukio la askari walioawa pale Mbande CRDB,
uvamizi wa NMB Mkuranga, Access bank Mbagala, kule Kibiti ambapo askari 8
waliuawa na silaha kuchukuliwa", amesema Kamanda Mambosasa
Kamanda Mambosasa aliendelea kusema kwamba baada ya jambazi huyo
kukamatwa alihojiwa na kutaja baadhi ya wahalifu anaosaidiana nao kwenye
uhalifu, na baada ya kumaliza kumuhoji alichukuliwa kuwahishwa
muhimbili na kufariki dunia akiwa njiani.
Post a Comment
karibu kwa maoni