Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Mobile Tz ametuletea zawadi nzuri watanzania
wote wapenda Burudani.
Baada ya kutoa Kitasa kisha Washa Tv na kuonekana kutofanya
vyema,safari hii hapa ameamua kuumiza kichwa zaidi na kujua kuwa mashabiki wake
wanapenda kitu gani.
Akizungumzia wimbo wake mpya Mobile ameuambia mtandao wa
Walter Habari kuwa wakati anaingiza mashairi akiwa studio alijua kabisa kile
anachokiimba kitagusa hisia za watu wengi.
Alisema ni wimbo alioumuza Kichwa usiku na mchana kwamba
aandike mashairi gani na yenye ujumbe wa aina gani huku akitafakari ni nani
atakayemshgirikisha kwa kuwa nyimbo zake mbili zilizopita yaani Kitasa na Washa
Tv hakumshirikisha yeyote.
Mkali huyo wa miondoko ya R&B ndani ya wimbo mpya unaojulkana kwa jina Tell
me yaani niambie amemshirikisha mkali wa michano ya Hip hop Racka Rymes lengo
ni kuwaletea burudani na ladha tofauti mashabiuki wa muziki wake.
Awali allipanga kufanya na Drizzy lakini baadae akaona pia
Racka naye anafaa kwenye wimbo huo japo anao mpango wa kufanya kazi nyingine na
Drizzy.
Post a Comment
karibu kwa maoni