Mkuu
wa majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amefunguka na
kusema kuwa vyombo vya Ulinzi na usalama vinakabiliana na matukio ya
uhalifu yanayotokea nchini kadili yanavyojitokeza na kusema kuwa
anaimani uhalifu huo utakwisha.
Mabeyo
amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kudai
kuwa kwa sasa wanataka kujiridhisha kuwa silaha hizo zinazotumika na hao
wahalifu zinatoka wapi na watu hao wasiojulikana ni watu wa aina gani,
hivyo amewataka wananchi kuviachia vyombo vya ulinzi na usalama vifanye
kazi yake.
"Haya
matukio tunaendelea kukabiliana nayo kama yale matukio ya Kibiti,
kwanini matukio ya Kibiti hayaleti mshtuko mkubwa sana sasa wakati watu
waliothirika ni wengi zaidi kuliko matukio ya sasa?
"Mimi
sitaki kuingia huko lakini nasema vyombo vya ulinzi na usalama wakati
wote vinakabiliana na matukio kadili yanavyojitokeza na ninaamini hali
itakuwa shwali na sasa vinashughulika."
"Hoja ya msingi tunataka kujiridhisha silaha hizi zinatoka wapi? Hawa watu ni wa aina gani,sasa vyombo mviachie vifanye kazi yake msitoa majibu haraka" alisisitiza Mabeyo
Katika
hatua nyingine,Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF),
Jenerali Venance Mabeyo ametoa tahadhari kwa wananchi kwamba kuna
matapeli wanaojifanya wanaajiri vijana kujiunga na jeshi.
Amesema
watu hao wanadai fedha ili kuwasajili vijana na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ), jambo ambalo ni kinyume na taratibu za jeshi kuajiri
vijana kwa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Mabeyo
ameonya kwamba mtu yeyote atakayetapeliwa na watu hao basi naye
atahesabika kama mmoja wa watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na
kuchukuliwa hatua mara moja.
"Maongezi
ya mtu na mtu hatuyatambui, ukitapeliwa nyamaza kimya kwa sababu
ukilalamika kwetu na wewe utachukuliwa kama sehemu ya watoa rushwa,"
amesema Jenerali Mabeyo.
Mkuu
huyo wa majeshi amebainisha njia mbalimbali ambazo wanazitumia kuajiri
vijana jeshini kuwa ni kuwachukua wale waliopitia mafunzo ya JKT au pale
wanapotaka watu wenye taaluma adimu kama vile madaktari, wahandisi au
wanasheria.
Amebainisha
kwamba jeshi linapokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na
wanachukua hatua kila wanapopata taarifa ikiwa ni pamoja na kuwatafuta
wahusika na kuwakamata.
"Kuna
mmoja alikusanya vijana 15 na kila kijana akatakiwa kulipa Sh1 milioni.
Aliwapangia chumba sehemu kisha akatoweka," amesema Mabeyo na
kusisitiza kuwa wengi wanaofanya vitendo hivyo ni raia, wanajeshi ni
wachache na wanachukuliwa hatua za kinidhamu mara moja
Post a Comment
karibu kwa maoni