Ni stori ya kweli iliyomtokea binti mmoja wa kabila la Iraq
[Mmbulu] amabye alipata mimba kabla ya kuolewa ndipo familia ikamtenga
ikiaminika kuwa kupata mimba wakati bado hujaolewa ni laana,wazee waliamua
kumtenga binti huyo ajulikanaye kwa jina la Imbori kisha kumtelekeza pori lenye
wanyama wakali ili amalizwe kabisa.
Lakini kijana aliepatia mimba ambaye hakutajwa na binti wala
hakujitokeza anayejulikana kwa jina la Mayo alijua kilichotokea akaamua
kumfuata binti huyo na kumwokoa hatimaye kwenda naye mpaka eneo lililojulkana
kama Imboru enzi hizo kabla ya sasa kuitwa Mbulu ambayo ni wilaya iliyopo
mkoani Manyara. Mbulu ndio sehemu inayotajwa kuwa na wasichana warembo wa
kuvutia.Stori hii Inakadiriwa kuwa ni zaidi ya miaka 500 iliyopita.
Kitila ameumiza sana kichwa kuutunga wimbo huu ulioturudisha mpaka miaka ya sasa ikisisitiza Msamaha na kuheshimu wazazi huku tukiishi kwa kumtegemea Mungu
Wimbo wenyewe huu hapa tuusikilize ameimba kwa hisia sana
msanii anayefanya vizuri kwenye muziki huu wa kizazi kipya Tanzania BOY KITILA.
Post a Comment
karibu kwa maoni