Wanachama
wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mbeya mjini, wametishia kutotoa ushirikiano
kwa Mwenyekiti mpya wa UVCCM, Stephano Halinga, aliyeshinda uchaguzi
mwishoni mwa wiki kwa madai kuwa mchakato wa kumpata Mwenyekiti huyo
ulikuwa na shinikizo.
Wakizungumza
mara baada ya uchaguzi huo, baadhi ya wanachama hao ambao hawakuwa
tayari kutaja majina yao walizielekeza lawama zao kwa Katibu wa UVCCM,
Gerald Kinawiro na Katibu wa CCM Mbeya Mjini, Gerald Mwadallu kuwa
walihusika na uteuzi wa Mwenyekiti mpya.
Akijibu
tuhuma hizo Katibu wa UVCCM, Mbeya Mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa
uchaguzi, Gerald Kinawiro, amedai kuwa, mchakato wa kuwapata wagombea
unafanywa kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama, hivyo hujuma hizo
hazina ukweli wowote na kama kuna mwanachama yeyote mwenye malalamiko
afike kwenye ofisi za chama.
Katika
kiny’ang’anyiro cha kumpata Mwenyekiti wa UVCCM Mbeya mjini Stephano
Halinga alipata kura 178, Farida Ngoyi kura 61 na Omari Omari kura 60.
Post a Comment
karibu kwa maoni