0
Wakulima wa zao la mbaazi mkoani Manyara wamelalamikia kuporomoka kwa soko la zao hilo mkoani hapa kwani  kwa sasa  hali si shwari katika soko kwakuwa  kwani kilo moja ya mbaazi inanunuliwa kati ya shilingi 300 na 400 tofauti na mwaka jana kilo iliuzwa kwa shilingi 2000 mpaka 2500.

 WALTER HABARI ilipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wakulima na walikuwa na haya ya kuzungumza.

Mbali na hilo mkuu wa idara ya kilimo na washirika BWN DANIEL LUTHER amewataka wakulima wa zao la mbaazi mkoani hapa kulitumia zao hilo kama zao la chakula na si zao la biashara kama ilivyo zoeleka kwa wengi. pia, amewataka wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji kujenga viwanda vya ubanguaji hususani kwa zao la mbaazi ili kuzalisha na kuuza bidhaa zitokanazo na zao hilo na si kuuza na kupeleka mazao nje ya nchi.

 Licha ya Tanzania kuwa na maeneo makubwa ya uzalishaji wa mazao ,India ndio wazalishaji na wanunuzi wakubwa wa zao la mbaazi duniani kutokana na wao kulitumia zao hilo kama chakula.

Hata hivyo kukosa soko katika zao hilo sokoni inasemekana inatokana na nchi ya India kwa mwaka hhuu kuzalisha kwa wingi Mbaazi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top