0
http://www.fikrapevu.com/wp-content/uploads/2017/02/wanafunzi.jpgJumla ya watahiniwa 29,221 wakiwemo wavulana 13,461 na wasichana 15,760  wanatarajiwa kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi katika Mkoa wa Manyara.
Afisa Elimu Taaluma Mkoa Lago Sillo, alisema kuwa watahiniwa hao wanatoka katika Wilaya za Kiteto,Simanjiro, Hanang’, Mbulu  na Babati na kwamba idadi hiyo inahusisha watahiniwa wenye mahitaji maalum ya uoni hafifu, viziwi na wasioona.
Alieleza kuwa  idadi ya watahiniwa kwa mwaka huu imeongezeka  kwa watahiniwa 2982 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo watahiniwa walikuwa 26,239 wavulana wakiwa 11,737 na wasichana 14,502.
Akizungumzia kuhusu maandalizi ya mitihani hiyo inayofanyika leo  Sillo alibainisha kuwa maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni ufanyaji wa mitihani  ambapo aliwataka wasimamizi wa mitihani kutenda haki kwa kufuata kanuni na taratibu za usimamizi wa mitihani.
Alifafanua kuwa wanafunzi  wanafunzi 8,471 wakiwemo wavulana 5,357 na wasichana 3,114  sawa na asilimia 22.4 wameshindwa kufanya mitihani  kutokana na mdondoko wa elimu.
“Mdondoko huo wa wanafunzi  umesababishwa na utoro, kuhama hama kwa jamii ya kifugaji hasa katika Wilaya ya Kiteto ambapo kumekuwa na asilimia 40 ya utoro” alisema Sillo.
Alisema suala la mdondoko  wa elimu  katika jamii ya kifugaji ni la mtambuka kwa kuwa jamii hizo hazitaki watoto wao wasome na badala yake wachunge mifugo pamoja na matatizo ya kifamilia.
Alifafanua kuwa wanafunzi walioanza darasa la kwanza  na wanaotarajiwa kuhitimu  katika Wilaya ya Simanjiro ni wanafunzi 3,598 , Mbulu mji 2,952,Mbulu vijijini 3.919, hanang’6,281,Babati Mji 2,179 na Babati Vijijini 6,946

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top