0






Mkuu Wa Progamu Ya Kufuatilia Uboreshaji Wa Elimu Nchini
Kupiitia Shirika La Haki Elimu Bw Godfrey Bonaventure Amesema Walimu Wakuu Wa
Shule Nchini Wamekuwa Chanzo Kinachokwamisha Malengo Ya Serikali Ya Kuboresha
Elimu Kupitia Fedha Za Ruzuku Ya Serikali Chini Ya Utekelezaji Wa Sera Ya Elimu
Bila Ya Malipo Kwa Kushindwa Kupeleka Fedha Hizo Kwenye Malengo Na Badala Yake
Wamekuwa Wakizipeleka Kwenye Michezo.
Bw Boneventure Ameyasema Hayo Mjini Babati Kwenye Siku Ya
Uwasilishaji Wa Taaarifa Ya Ufuatiliaji Wa Fedha Za Umma Hususani Fedha Hizo
Zinazotolewa Kulingana Na Idadi Ya Wanafunzi Shuleni Uliofanywa Na Marafiki Wa
Elimu Kwa Baadhi Ya Shule Za Halmashauri Ya Mji Na Wilaya Ya Babati Kunakosababishwa
Na Baadhi Ya Walimu Kutofahamu Muongozo Huo.
Nao Baadhi Ya Walimu Wakuu Wakizungumzia Changamoto Ya
Kuacha Kutumia Fedha Hizo,Wameeleza Kuwa Ni Migogoro Kati Yao Na Kamati Za
Shule Mazingira Ambayo Yanasababisha Kushindwa Kukarabati Majengo Ya Shule
Aidha Kusababisha Kushusha Kiwango Cha Elimu,Hatua Ambayo Mkuu Wa Wilaya Ya
Babati Mhandisi Raymond Mushi Akikiri Baadhi Ya Walimu Hawazingatii Muongozo.
Hata Hivyo Marafiki
Hao Wa Elimu Licha Ya Kugundua Changamoto Hiyo Wameiomba Idara Ya Elimu
Kufuatilia Ili Kuokoa Kiwango Cha Elimu Kisishuke Tofauti Na Malengo Ya
Serikali.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top