0






Uchaguzi wa
mwenyekiti wa Ccm wilaya ya Babati vjijini  uliovurugika 
ijumaa ya wiki iliyopita kutokana na wagombea kushindwa kufikisha nusu
ya kura,sasa umepangwa kurudiwa tena  jumanne ya  kesho  oktoba 10 2017.
Hatua hiyo ilizua malumbano kati ya wajumbe ambao walibaki
kusubiri matokeo mapaka majira ya saa saba za usiku hali iliyomfanya mkurugenzi
mkuu kutaka uchaguzi urudiwe lakini idadi ya wajumbe ikawa pungufu.
Katibu Ccm wilaya ya babati vijijini Edna Edmund ambaye
ndiye mkurugenzi wa uchaguzi  akatangaza
uamuzi wa kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Martha Umbura aliwataka
wajumbe wawe watulivu wakati wanasubiri uchaguzi nafasi ya mwenyekiti kurudiwa.      zi
Uchaguzi wa chama hiko chenye   mashina zaidi ya laki 2 na 22 elfu na matawi
zaidi ya 23 elfu nchi nzima
 unafanyika  katika  ngazi ya mashina na matawi na kata.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top