0







Gharos Riwa  & Thomas Masalu - BUNDA

Mkuu wa mkoa wa Mara Dr. Charles Mlingwa ameipongeza Halmashauri ya mji wa Bunda kwa kuonyesha utayari wa kujenga kiwanda cha nyama ndani ya halmashauri yao ambapo amesema ni moja ya hatua kubwa ambayo itasaidia kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Dr.Mlingwa ametoa pongezi hizo leo wakati akikagua eneo litakalojengwa machinjio ya kisasa na kiwanda cha kusindika nyama  katika kata ya Bunda stoo Halmashauri ya mji wa Bunda.

Dr.Mlingwa amesema anataka kuona kiwanda cha nyama kinaanzishwa ndani ya mkoa wa Mara hivyo amesema kwa kuwa Halmashauri ya mji wa Bunda wameonyesha nia ya kuanzisha kiwanda hicho ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kakamilisha mradi huo.


Hata hivyo Dr.Mlingwa amesema anafahamu kuwa wapo wananchi watakao hitaji fidia kupisha mradi huo hivyo amewaomba waondoe shaka na kwamba kila mtu atapata haki yake kwa wakati bila shida yeyote na kuwataka kuanza maandalizi ya kupishisha eneo hilo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top