0
Watumishi wa Umma na watanzania kwa ujumla  wametakiwa kuwa na mazoea ya kupima afya zao
mara kwa mara ili kujitambua na kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoani
Manyara  Hamisi Malinga amefungua
rasmi kampeni ya kupima Ukimwi na Magonjwa sugu 
yasiyo ambukiza mahali pa kazi kwa watumishi wa Umma Halmashauri ya
wilaya ya Babati.
Akizungumza wakati wa kufungua zoezi la upimaji wa virusi
vya ukimwi na magonjwa yasiyoambukiza kwa watumishi wa Umma  halmashauri ya wilaya ya Babati  leo Mkurugenzi 
mtendaji wa wilaya Hamisi Idd Malinga 
ameeleza kuwa hatua hiyo ni wito wa serikali inayowataka watumishi wote
kupima  kwa hiari na kujua afya zao.
Malinga amesema kwa kuzingatia mchango wa watumishi wa Umma
kwa maendeleo ya Babati na Taifa udhibiti wa magonjwa haya mahala pa kazi unahitaji
kupewa msukuomo wa kipekee ili kunusuru afya zao na kuiwezesha nchi kufanikiwa
katika azma yake ya Tanzania ya viwanda.
Akizungumzia kamati ya UKIMWI ya Wilaya ya Babati iliyoundwa
mwaka 2007 afisa utumishi wilaya Bi Veronika Mana  amesema iliibua magonjwa sugu yasiyoambukiza
ambayo yamekuwa tatizo kwa jamii wakiwemo watumishi wa umma.
Naye mwenyekiti wa kamati ya Ukimwi ambaye pia ni muathirika
waugonjwa wa  Ukimwi Mwanahamisi  Athumani Said Maige amewataka watumishi kupima
afya zao bila woga na wakigundulika waanze kutumia dawa mapema.
Amesema kwa sasa tangu agundulike na ugonjwa huo ni miaka
ishirini na tano sasa na anaendelea na kazi zake kama kawaida.
Mimi mwanzoni niliteseka sana kwa kunyanyapaliwa na watu ila
tangu nianze kutumia dawa afya yangu inazidi kuimarika.


Nilikuwa ninazaa watoto wanakufa bila kujua sababu ni
zipi,nilivyopatiwa ushauri na wataalamu wa afya nikazaa watoto wawili mpaka
sasa mmoja wa kike yupo na familia yake na mwingine ni mwanafunzi.


Ukiwa wazi ukimwi haukutesi ila ukilala nao utakutesa na
utashindwa kufanya kazi zako kwa sababu utakuwa unawaza  kala mara,hivyo jitokezeni mjue afya
zenu.alisistiza Bi Mwanahamisi.


Aidha anasema wapo vijana wengi wa kike na wa kiume wazuri
wanaishi na ugonjwa huo hivyo ni vyema kuwatambua ili kuinusuru jamii dhidi ya
usambazaji wa ugonjwa huo hatari.
Naye mganga mkuu wa wilaya ya Babati Dr.Madama Hosea amesema
katuka kampeni hii ya kupima afya litafanyika katika vituo vyote vya afya
vilivyopo wilaya ya Babati kwa watu wote bila malipo hadi novemba 15 mwaka huu.
Takwimu  za shirika la
umoja wa mataifa na wizara ya afya inaonyesha kuwa asilimia 27 ya watanzania
wana tatizo la shinikizo la damu na asilimia 9 wanaugua kisukari huku athari
zake zikionekana kuwa kubwa.
Pia utafiti huo unaonyesha kuwa magonjwa ya moyo,Kisukari
yanaweza kuzuilika kwa asilimia 80 na saratani asilimia 50 kwa kuwa na na
mtindo bora wa maisha unaozingatia ulaji wa vyakula.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top