0
Timu ya Netiboli Toto Africa.
Makamu Mwenyekiti wa chama cha mpira wa wanawake Tanazania
[CHANETA] Mheshimiwa Anna Gidarya mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara
[CHADEMA] amesema  atahakikisha mkoa
unapata timu imara itakayoshiriki  ligi
mbalimbali kitaifa.

Timu ya Netiboli Galapo Quens
Anna Gidarya ameyazungumza hayo baada ya kufungua mashindano
ya netbaal mjini Babati katika uwanja wa Kwaraa kutafuta wachezaji watakauwakilisha
mkoa wa Manyara kitaifa.

Mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema akifungua
michezo hiyo ya Netball amewataka wachezaji hao wawe na nidhamu ili kuweza
kupata ushindi huku wakimtanguliza Mungu.
Timu ya Netiboli Rift Valley
Timu nne zilizojitokeza zote zinatokea Babati vijijini ,timu
hizo ni Galapo Quens,Toto Africa,Chem Chem pamoja na Rift Valley.

Afisa utamaduni na michezo mjini Babati Fabian Manda
amemsifu Mbunge huyo na kuahidi kushirikiana nae.
Timu ya Netiboli Chem chem

Tarehe 23 oktoba mwaka huu, Uongozi wa Zamani wa Chama cha
Netiboli Tanzania (CHANETA) chini ya mwenyekiti wake mstaafu Mama ANNA FAITH
KIBIRA umekabidhi ofisi kwa viongozi wapya wa chama hicho kinachoongozwa na
mwenyekiti mpya Devotha John Marwa akishirikiana makamu mwenyekiti  Anna Gidarya ,makabidhiano yaliyofanyika
katika ukumbi wa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake mwenyekiti mpya wa CHANETA Dokta DEVOTHA
JOHN MARWA ameushukuru uongozi uliopita kwa kazi nzuri na hatua ambayo wamepiga
katika kuendeleza mchezo wa netiboli nchini Tanzania.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top