0


Image result for mwigulu nchembaWaziri wa mambo ya ndani Mwigulu Lameck Nchemba  ametembelea nyumba za askari polisi zinazojengwa mkoani  Arusha  baada ya kuteketea kwa moto na kuwapongeza wananchi kwa kujitolea kuwachangia fedha ili wapate makazi mapya.
Hivi karibuni jeshi la  polisi jijini Arusha lilipata pigo baada ya Familia  13 zenye watu 44 kuunguliwa nyumba zao katika mtaa wa Sekei.
Akizungumzia hali ya usalama nchini Mwigulu amesema kila anaetenda maovu lazima akamatwe na kwamba hakuna muhalifu popote pale atakaebaki salama.
Waziri Nchemba amefika jijini Arusha akitokea mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwenye ufunguzi wa maazimisho ya wiki ya nenda kwa Usalama Bara barani kitaifa  yaliyofunguliwa na makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top