0


Image resultImeeleza kuwa wananchi wengi wanakosa haki zao kutokana na uelewa mdogo kuhusu sheria jambo linalosababisha ukatili, unyanyasaji kwa wanawake  katika migogoro mingi ya familia .

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Kituo cha usaidizi  wa kisheria Wilayani Mbulu (MPAC) Ezekiel Assecheck  wakati akizungumza na Gazeti hili ofisini kwake ambapo alisema kwamba wanawake wengi wamekuwa  wakifanyiwa ukatili  huku wakiwa hawajui pa kwenda kupata haki yao.

Alisema kuwa Kituo hicho  juni 2017  kilipokea  kesi 15 zilizopata suluhisho kati ya hizo  13 zilihusu wanawake waliokuwa wakikabiliwa namatatizo ya migogoro ya ardhi lakini pia na migogoro ya kifamilia.

“Dhamira ya Kituo chetu  ni kuiwezesha jamii kufahamu sheria na wajibu wa kutetea haki wakati wote kwa kutoa elimu ya sheria ili wananchi watumie katika kuleta maendeleo” Alisema Assecheck.

Aidha kituo hicho kimeweka mkakati wa kufundisha  sheria katika mikutano ya hadhara inayohusu masuala ya ndoa, ukatili na migogoro ya ardhi kusuluhisha kesi zinazojitokeza za mtu mmoja mmoja na vikundi.

Hata hivyo kituo hicho kimeweza kuwafikia wananchi zaidi ya 800 kwa mwezi Agasti na kuwapatia elimu na msaada wa kisheria .

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top